MENEJA wa klabu ya Liverpool Rafa Benitez amethibitisha kupokea offer kutoka katika vilabu mbalimbali zenye lengo la kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo toka nchini Hispania Fernando Torres.Benitez amevitaja vilabu vilivyotuma offer zao huko Anfiled ni pamoja na Chelsea, Manchester City, Manchester United na klabu ya Real Madrid
Aidha amewataja viungo wake Xabi Alonso na Javier Mascherano pia wameemdelea kuwa kwenye mtiririko wa kutakiwa na baadhi ya vilabu barani ulaya .
Hata hivyo licha ya kupoke offer hizo Benitez amethibitisha kuwa msambuliaji Torres ndiye aliyeonyesha nia ya kuendelea kubaki Anfield kwa msimu ujao.
Benitez ametoa wito kwa baadhi ya vilabu na kutaka vifahamu kwamba klabu hiyo ina kikosi imara na lengo la klabu hiyo ni kutaka kukiimarisha kikosi hicho, hivyo hawana mpango wa kuwauza baadhi ya wachezaji wao walio bora .
No comments:
Post a Comment