Meneja wa klabu ya Barcelona Pep Guardiola, ameliorodhesha jina la mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon Samuel Eto'o katika orodha ya wachezaji atrakaowauza katika kipindi hiki cha usajili.Pep Guardiola ameliorodhesha jina la mshambuliaji huyo, huku kukiwa na taarifa za kuwepo uwezekano wa Eto’o kuelekea Gueisepe Meaza yalipo makao makuu ya klabu ya Inter Milan ambayo ipo tayari kumtoa Zlatan Ibrahimavic kuelekea huko Nou Camp kama sehemu ya kubadiolishana.
Akizungumzia hatua hiyo Pep Guardiola amesema umewadia wakati wa mshambuliaji huyo kuondoka klabuni hapo na kuwapisha wachezaji wengine kuleta changamoto tofauti za kiushindani hususan katika safu ya ushambuliaji.
Amesema mashabiki wengi wa klabu ya Barcelona ulimwenguni kote anajua watamueleza tofauti huku wengine watamjadili kwa kueleza kuwa amefanya makosa ya kutarajia kumuuza mshambuliji huyo lakini akaendelea kusisitiza kwamba safu yake ya ushambuliaji inahitaji changamoto tofauti.
Pep Guardiola ambae ni meneja aliepata mafanikio makubwa katika kipindi cha msimu mmoja aliokuwepo huko Nou Camp ametanabai halitokuwa jambo la muhimu kutomshukuru Eto’o kwa msaada mkubwa alioutoa klabuni hapo katika michuano mbali mbali hususan ile ya ligi ya mabingwa barani ulaya na katu kwa hilo hawatomsahau.Itakumbukwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita mshambuliaji huyo alionyesha dalili za kutokuwa tayari kuondoka klabuni hapo licha ya klabu ya Manchester City kuonyesha nia zote za kumuhitaji, kwa kudai kwamba anahitaji asilimia ya fedha za usajili wake kama mkataba unavyoagiza.
Samule Eto’o alisajiliwa na klabu ya Barcelona mnamo mwaka 2004 akitokea katika klabu ya Real Mallorca kwa ada ya uhamisho wa paund million 16.
No comments:
Post a Comment