
Beki wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu na klabu ya Everton Joleon Lescott anatarajia kupelekea maombi ya kutaka auzwe kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Bill Kenwright.
Beki huyo amepelekea maombi hayo kwa lengo la kujirahisishia njia ya kuelekea huko City Of Manchester yalipo makao makuu ya klabu ya Manchester City.
Beki huyo tayari ameshawekwa katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na meneja wa Man city Mark Hughes ambae alishamtengeza kiasi cha paund million 15-18.
Hata hivyo meneja wa klabu ya Everton David Moyes tayari ameshaweka msisitizo wa kutokuwa tayari kumuuza beki huyo kwa kisingizio cha kutata kuendelea kuwa kikosi chake ambacho msimu uliopita kilipigana kufa na kupona katika michuano ya ligi kuu na kumaliza katika nafasi ya tano.
No comments:
Post a Comment