
Uongozi wa klabu ya Everton umethibitisha kuanza kwa mazungumzo kati yao na beki wa kimataifa toka nchini Uswis pamoja na klabu ya Arsenal, Philippe Senderos.
Pamoja kuathibitishwa kwa taarifa hizo, uongozi huo wa The Toffees umesema bado bei ya kuuzwa kwa mchezaji wao haijazungumzwa kati yao na uongozi wa klabu ya Arsenal.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 anatarajia kusajiliwa na Everton kwa lengo la kuziba nafasi ya Joleon Lescott aliejiunga na klabu ya Man City.
No comments:
Post a Comment