KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 4, 2009




Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Misri Ahmed Hossam Hussein Abdelhamid Mido amekamilisha mipango ya kurejea nyumbani kwao kuichezea klabu yake ya zamani ya Zamalek.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anarejea nyumbani kuicheza klabu hiyo aliyoakuwa akiitumikia kati ya mwaka 1999-2000, baada ya kukubaliwa na uongozi wa klabu ya Middlesbrough ya nchini Uingereza.

Hata hivyo Mido anarejea nyumbani kwa makubaliano ya kuuzwa kwa mkopo katika klabu yake za zamani ya Zamalek.

Mido alisajiliwa na Middlesbrough mwezi August mwaka 2007 akitokea katika klabu ya Tottenham kwa gharama ya paund million 6.

No comments:

Post a Comment