Kipa wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu bingwa nchini Uingereza Manchester United Edwin van der Sar atalazimika kuikosa michezo ya mwanzo ya msimu mpya wa ligi baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo katika kidole cha mkono wa kushoto.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 38, anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manane ambapo imeaminika muda huo atakuwa amepona kisawa sawa na kurejea kikosini.
Van der Sar alivunjika kidole hicho alipokuwa katika purukushani za kuzuia mikwaju ya penati kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Audi, ambapo Man utd walifungwa kwa mikwaju 7-6 na Bayern Munich.
Mchezo huo uliunguruma kwenye uwanja wa Allianz Arena huko nchini ujerumani kati kati ya juma lililopita.

No comments:
Post a Comment