
Meneja wa klabu ya Man City Mark Hughes amemtaka kocha wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona kutomuita mshambuliaji wake Carlos Tevez.
Mark Hughes amesema halitokuwa jambo jema kwa kocha huyo kumuita Teves katika timu ya taifa ya Argentina ambayo inatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya taifa ya Urusi mnamo August 12.
Akitao sababu za kumtaka Maradona kutokumwita Tevez, meneja huyo wa Man City amesema mshambuliaji huyo aliemsajili siku kadhaa zilizopita anatakiwa kupumzika kwa sasa ili aweze kurejea katika kiwango chake cha kawaida, na hii ni kutokana na ziara waliyoifanya huko chini Afrika kuisni majuma mawili yaliyopita.
No comments:
Post a Comment