KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 13, 2009

AJALI MATEMBEZINI.


Mlinda mlango wa klabu ya Tottenham Hotspur Carlo Cudicini amepata maumivu makali mwilini mwake baada ya kupata ajali na pikipiki mashariki mwa jiji la London .

Cudicini amepata ajali hiyo baada ya pikipiki yake aina ya BMW kugongana uso kwa uso na gari ndogo na kupata maumivu mkononi na kiunoni ambapo bado taarifa za vipimo zinasubiriwa na uongozi wa klabu hiyo kutoka hospitalini alikolazwa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 36 alisajiliwa Spurs akitoka kwa mahasimu wao klabu ya Chelsea mwezi January mwaka huu kama mchezaji huru na tayari ameshacheza mechi 8 wakati kipa namba moja wa klabu hiyo Heurelho Gomes alipokuwa majeruhi .

Cudicini aliichezea klabu ya Chelsea kwa muda wa miaka 10 na pia amewahi kuzichezea klabu za AC Milan na Lazio za nchini kwao Italia.

Dereva wa gari lililogongana na pikipiki ya kipa huyo akikuwa mwanamke na kwa bahati nzuri yeye hakuumia pamoja na mwanae aliekua nae.

2 comments:

  1. da mwana web yako nomaa yaani naifagilia ki noma mtu wangu kaza hivyo hivyo yaani safi kwa habari za michezo na upo fasta kuziweka safi sana .

    ReplyDelete
  2. yani wewe unastahili sifa zote kabisaa,,kila litokealo michezoni lazima utupashe.Blog yako iko juu kiukweli.Ila siku moja weka picha yako tukufamu vizuli .Kaza misuli utafika mbali.

    ReplyDelete