Shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA, limeandaa mkutano maalum utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu nchini Afrika kusini kwa lengo la kujadili matukio mbalimbali ambayo yamejiri katika mchezo wa soka ndani ya siku kadhaa zilizopita.Agenda kubwa katika kikao hicho cha mwezi Disemba ni kutazama michezo ya kuwani nafasi ya kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Kwa muda wa juma zima mashabiki wa soka ulimwenguni kote wamekuwa wakimzungumzia mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry kwa kitendo chake cha kushika mpira kabla ya kutoa pasi iliyozaa goli lililofungwa na, William Gallas kwenye mchezo wa hatua ya mtoano dhidi ya jamuhuri ya Ireland.
Pia kikao hicho kitautazama mchezo mwingine kati ya Algeria dhidi ya Misri uliochezwa mjini Khartoum nchini Sudan na kushudia Algeria wakiibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Ajenda nyingine ambayo itazungumza na maafisa wa shirikisho hilo ni vitendo vya kutumia kamari kwa nia ya kushawishi matokeo ya mechi barani ulaya.
Isitoshe, shirikisho la kandanda la Iraq lilisimamishwa kwa muda kutokana na serikali kuingilia shughuli zake, kinyume na kanuni za Fifa.
No comments:
Post a Comment