KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 11, 2009

BARCELONA NA MAN CITY KUKAA MEZA MOJA.

Klabu ya BARCELONA imeonyesha nia ya kuridhia kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Manchester City Robinson Robinho kwa mkopo.

Uamuzi huo ulitarajiwa kufikiwa huko Abu Dhabi ambapo kikosi cha klabu ya Man City kimeweka kambi kwa ajili ya kujichua na muendelezo wa michuani mbali mbali inayowakabili.

Katika mkutano wa makubalino hayo huenda akawepo mkurugenzi mtendaji wa Man City Garry Cook, wawakilishi wa klabu ya Barcelona , baba yake mzazi Robinho na meneja wake Chris Nathaniel.

Ifahamike kuwa, Robinho anatarajia kuhamia Barcelona katika dirisha dogo la usajali itakapofika mwezi januari mwaka 2010 kwa mkopo huku akitarajiwa kusajiliwa moja kwa moja hapo baadaye.

Hata hivyo imeelezwa kuwa ili usajili huo ufanikiwe klabu ya Man City inataka irejeshewe kiasi cha paundi milioni 32.5 ilicholipa katika klabu ya Real Madrid miezi 15 iliyopita kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo.

Hata hivyo kusajiliwa kwa Robhino Man City hakujailetea mafanikio makubwa klabu ya Man City hatau mbayo imeonyesha ni vipi alivyokuwa na kila sababu ya kuondoka huko City Of Manchester.

Mpaka sasa Robinho amecheze michezo 32 akiwa na klabu yake ya Man City na kufunga mabao 14 na kwa sasa amekuwa nje ya uwanja kufuatia majuraha yanayomkabili.

No comments:

Post a Comment