KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 11, 2009

SABABU NI ARSENE WENGER.

Kiungo wa klabu ya Manchester United DARREN FLETCHER amesema anaadhibiwa na waamuzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kutokana na kauli aliyoitoa meneja klabu ya Arsenal Arsene Wenger mwezi September kumuhusu yeye.

Kauli hiyo Fletcher imekuja baada ya kuadhibiwa na mwamuzi Martin Atkinson na kupelekea klabu ya Chelsea kupata bao la ushindi dhidi ya klabu ya Manchester United katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.

Fletcher amesema kauli aliyoitoa Wenger imeanza kuathiri uamuzi wa waamuzi jambo ambalo ni la aibu baada ya kuadhibiwa na waamuzi bila sababu.

Itakumbukwa kwamba bosi huyo wa Arsenal aliwalaumu baaadhi ya wachezaji wa Man United kwa kucheza mchezo mbaya baada ya klabu yake kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao mawili kwa moja katika dimba la Old Trafford mapema msimu huu.

Fletcher anasema pamoja na kutotajwa jina wake katika maelezo ya Arsene Wenger bado maelezo hayo yalimuhusu hali iliyopelekea kuadhibiwa na waamuzi kila mara.

Hatua hiyo ya Fletcher ya kumlalamikia Wenger imekuja baada ya mwamuzi kuamuru upigwe mpira wa adhabu iliyosababishwa na kiungo huyo kwa kumchezea vibaya Ashley Cole na kupelekea bao la ushindi kupatikana katika mchezo dhidi ya MAN UTD na CHELSEA uliochezwa katika dimba la Stamford Bridge.

Kwa matokeo hayo Chelsea sasa inaongoza ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa tofauti ya point tano dhidi ya Arsenal walio katika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment