Wakati michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ikitarajiwa kuendelea tena hii leo, huko Nou Camp hofu imetanda kufuatia taarifa za Lionel Messi kuwa katika hali ya sintofahamu ya kucheza ama kutocheza mchezo dhidi ya Inter Milan.Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anafanyiwa uchunguzi kuhusiana na maumivu ya paja aliyopata mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Athletic Bilbao ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.
Kuumia kwa Messi kumekuja wakati tumu yake inamuhitaji zaidi ambapo mwishoni mwa juma hili, pia wanakabiliwa na pambano gumu na watani wao wa jadi Real Madrid.
Zlatan Ibrahimovic, Yaya Toure na Eric Abidal nao wnaatarajiwa kuwa nje ya kikosi hii leo kufuatia hali zao kutokua nzuri, lakini meneja wa Barcelona Pep Guardiola amesisitiza kuwachezesha wachezaji waliosalia kikosini.
Guardiola pia anasubiri taarifa za mlinzi Rafael Marquez, ambaye anafanyiwa uchunguzi wa homa ya mafua ya nguruwe iliyowapata Toure na Abidal.
Michezo mingine ya ligi ya mabingwa inayopigwa leo ni pamoja na;
AZ Alkmaar v Olympiakos
Arsenal v Standard Liege
Barcelona v Inter Milan
Debrecen v Liverpool
Fiorentina v Lyon
Rangers v VfB Stuttgart
Rubin Kazan v Dynamo Kiev
Unirea Urziceni v Sevilla
No comments:
Post a Comment