KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, November 24, 2009

ILIKUA ZAHMA KUBWA TURUDISHE KIINGILIO !!!


Wachezaji wa Wigan wamekubaliana kurejeshea viingilio mashabiki wao waliosafiri hadi jijini London kushuhudia mchezo wa ligi kuu kati yao na Tottenham ambao waliibuka na ushindi wa mbao tisa kwa moja.

Wachezaji wa Wigan wamefikia hatua hiyo baada ya kusononeshwa na hatua ya kufungwa, katika uwanja wa White Hart Lane ikiwa ni mabao mengi kufungwa katika Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza.

Nahodha wa Wigan Mario Melchiot amesema kupitia tovuti ya klabu hiyo, wachezaji kama kundi wanahisi wamewaangusha mashabiki wao hivyo hawana budi kuwarejeshea viingilio vyao.

Kufuatia kichapo hicho cha mwishoni mwa juma lililopita Wigan inakuwa klabu ya kwanza kufungwa mabao tisa katika Ligi Kuu ya soka ya nchini Uingereza ambapo kwa mara ya mwisho zahma hiyo iliwaangukia Ipswich town kwa kukubali kichapo cha mabao tisa kwa sifuri kilichotolewa na Man Utd mnamo mwaka 1995.

2 comments:

  1. Hii habari ilikuwa kama vile wenzao Totts walikuwa wakicheza kwa mikono nao Wigan wakaambiwa wacheze kwa miguu teh teh teh matokeo kama ya rugby bwana, kha.
    Viwanja: Asante sana mkuu kwa kulivalia njuga suala la michezo, ni blogu niliyojiandikisha kusoma kila unapobandika jambo kwa kuwa unahabarisha habari motomoto za hivi punde na kutupa fleva ya mambo yanayotokea katika viwanja vya soka na ulimwengu wa kandanda. Endeleza libeneke la anga la michezo.
    Shukran!

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee yuko juu kwa michezo,,kaza buti mheshimiwa,ukihalibikiwa vifaa vyako tufahamishe ilitusaidiane, blog yetu isiwe na tatizo.

    ReplyDelete