KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 12, 2009

BISINGWA NAE OUT !!!!!!!!!!!!


Imethibitika kuwa beki wa kimataifa toka nchini Ureno na klabu ya Chelsea Jose Bosingwa atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu ijayo kufuatia maumivu ya goti yanayomkabili.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 alipata maumivu hayo kati kati ya mwezi wa kumi mwaka huu na kwa mahesabu ataonekana tena uwanjani mwaka ujao.

Ikumbukwe kuwa beki huyo wa zamani wa klabu ya Fc Porto alijiunga na klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paund million 16.2 mwezi May mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment