
Mashabiki wa klabu ya Newcastle walio na hasira wanapanga mikakati ya kutumia jeshi la Polisi nchini Uingereza kumuondoa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley.
Mmoja wa mashabiki hao ambaye ni mkereketwa wa kweli wa klabu hiyo ambaye pia ni muimbaji maarufu nchini Uingereza Sting amesema anawaunga mkono mashabiki hao walio na mikakati ya kumfukuza mmiliki huyo ambaye anachukiwa kutokana na uamuzi wake wa kubinafisha jina la uwanja wa klabu hiyo la St James Park .
Mashabiki hao wameazimia kuinunua klabu hiyo kwa kuanzisha kampeini ijulikanayo kama Newcastle United Supporters Trust's Yes We Can ya kuinunua klabu hiyo.
Tayari jeshi la Polisi limeshamtumia taarifa mmiliki hiyo kusitisha mpango wake wa kubinafisha jina la uwanja wa klabu hiyo linalotaraji kujulikana kama sportsdirect.com@St James' Park.
Sting amesema akiwa kama shabiki wa maisha wa klabu hiyo asingependa kuona mabadiliko hayo na kinachotakiwa ni kudumisha utamaduni wa klabu hiyo.
Kampeini hiyo inatarajia kudumu kwa muda wa majuma sita kuhamasiha mashabiki waweze kumiliki klabu yao .

Kampeini hiyo itahusisha mazungumzo na wawekezaji waliona na nia ya kuendelea kuwekeza katika klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kutaka ushauri wao kuhusu mashabiki wenyewe kumiliki klabu yao.
No comments:
Post a Comment