
Meneja wa klabu ya Manchester City Mark Hughes ametoa nafasi kwa mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Brazilia Robinho kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa wa Novemba 21 dhidi ya klabu ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu toka mwezi Sepetemba mwaka huu ambayo aliyapata kwenye mchezo wa kuwani nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia katika ya Brazil na Argentina.
Hata hivyo imeelezwa kuwa tayari Robinho ameanza mazoezi na wachezaji wenzake huko Abu Dhabi walipoweka kambi kwa sasa huku akitarajia kujiunga na timu yake ya taifa ya Brazil ambayo itakua na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uingereza mnamo Novemba 14 huko nchini Qatar.
No comments:
Post a Comment