KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 12, 2009

CROUCH ANASWA DISKO.


Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Peter Crouch amesema anajutia uamuzi wake wa kwenda disco baada ya kupigwa picha na mapaparazi hatua ambayo ilimemsababishia kulaumiwa na meneja wake Harry Rednap ambaye amewapiga marufuku wachezaji wake kwenda katika kumbi za starehe.

Mshambuliaji huyo alikutwa na kadhia hiyo akiwa na mchezaji mwenzake Jonathan Woodgate baada ya kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Portsmouth hatua ambayo inaweza kumuharibia kwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello .

Crouch anasema meneja wake Rednap alidiriki kumuita mjinga na kumueleza kuwa anachezea bahati yake ya kuitwa katika kikosi kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia iwapo hataacha tabia yake ya kwenda katika kumbi za starehe ambapo amemshauri kufanya hivyo baada ya fainali hizo iwapo atajumuishwa katika kikosi hicho.

Crouch amesema huenda skendo hilo likamuudhi Capello ambaye anakiandaa kikosi kitakachotajwa kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Africa Kusini.

Licha ya kuwa na wasiwasi hio Crouch bado hajalaumiwa na Capello licha ya kufahamu kwamba huwa wanaruhusiwa kusherekea ushindi wa timu ya taifa wakiwa pamoja na sio mchezaji mmoja mmoja wakiwa katika timu ya taifa.


Mshambuliaji huyo ana rekodi nzuri ya ufungaji mabao ambapo katika timu ya taifa amefunga mabao 16 katika michezo 17 aliyoichezea timu ya taifa lake la Uingereza licha ya kuwa amekosolewa kwamba huwa anafunga mabao hayo wakati timu hiyo inapokuwa inacheza na timu nyepesi au zisizokuwa na uwezo mkubwa.

No comments:

Post a Comment