KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 11, 2009

REAL MADRID KAMA LIVERPOOL !!!!!!!


Mabingwa wa zamani wa nchini Hispania wenye ndoto za kurejea zama zao za kufanya kweli msimu huu, Real Madrid usiku wa kuamkia leo walitupwa nje ya michuano ya Copa del Rey baada ya kukanyagwa mabao manne kwa moja na klabu ya Alcorcon.

Madrid wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa kurejesha mabao manne waliyokuwa wamefungwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa majuma mawili yaliyopita na klabu ya Alcorcon ambayo jana ililala kwa bao moja kwa sifuri.

Madrid wametupwa nje huku wakiwa na kikosi kilichosheheni wamchezaji kama Kaka, Raul pamoja na Ruud van Nistelrooy huku bao pekee katika mchezo huo likifungwa na Rafael van der Vaart.

No comments:

Post a Comment