Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Didier Drogba ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo itakamilisha ratiba ya kuwani nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 mwishoni mwa juma hili dhidi ya timu ya taifa ya Guinea.
Mshambuliaji huyo ameachwa katika kikosi hicho kufuatia majaraha aliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man Utd.
Drogba mwenye umri wa miaka 31 aligongwa sehemu za kifua na beki wa klabu ya Man Utd Jonny Evans.
Hata hivyo mshambuliaji huyo huenda akajiunga na kikosi cha timu ya taifa lake kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani ambao unatarajia kuchezwa kati kati ya juma lijalo.

No comments:
Post a Comment