KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 11, 2009

MSIBA WA WANASOKA.

Kipa wa kimataifa toka nchini Ujerumani na klabu ya Hannover 96 Robert Enke amefariki dunia baada ya kugongwa na treni.

Taarifa iliyotolewa na Polisi nchini Ujerumani zimeeleza kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 amefikwa na umauti kwa kusudio la kujiua huko kaskazini magharibi mwa mji wa Hannover.


Katika uhai wake Robert Enke aliwahi kuichezea timu ya taifa lake la Ujerumani mara nane na kwa upande wa vilabu amevichezea vilabu vya Carl Zeiss Jena, Borussia Mönchengladbach, Benfica, Barcelona, Fenerbahce na Tenerife, kabla ya kurudi ligi ya Bundesliga akiwa na Hannover mwaka 2004.

Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kimetoa taarifa za kusikitishwa na kifo cha Robert Enke.
Nae meneja wa timu ya ujerumani Oliver Bierhoff ameongeza kuwa wamshtushwa sana na kifo cha kipa huyo na kufikia hatua ya kukosa la kusema chochote.

No comments:

Post a Comment