
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Croatia na klabu ya Arsenal Eduardo amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kusalia Ashburton Grove.
Eduardo amesaini mkataba huo huku akiwa anahusishwa na taarifa za kutakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Liverpool ambayo kwa sasa inakwenda mzobe mzobe kwenye michuano kadha wa kadha barani Ulaya.
Akizungumzia hatua ya kusaini mkataba wa mshambuliaji huyo, meneja wa klabu ya Arsenal Arsene wenger, amesema Eduardo ni mchezaji anaetazama mbali katika maisha yake ya soka na ndio maana amekubali kuendelea kusalia huko Emirates.

No comments:
Post a Comment