Klabu ya Tottenham Hotspours inajipanga kumsajili mlinda mlango wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Manchester United Ben Foster kwa ada ya paundi milioni 6 ifikapo mwezi January mwaka 2010.Kipa huyo wa Manchester United amekiri huenda akaihama klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford baada ya kuwa kipa wa tatu katika kikosi cha babu.
Tayari meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp ameshatangaza kuingia sokoni kwa lengo la kumsajili kipa mpya ambae atakua mbadala wa kipa wake namba mbili Carlo Cudicini aliepata ajali ya pikipiki juma lililopita .
Foster anafikiria uamuzi wa kuondoka Old Trafford ili aweze kujihakikishia nafasi ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini mwaka 2010.
Foster mwenye umri wa miaka 26 alicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Brazil ambapo Uingereza walikubali kichapo cha bao moja kwa sifuri.
No comments:
Post a Comment