KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, November 24, 2009

JINAMIZI LAMUANDAMA HENRY.


Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry anafikiria kuacha soka la kimataifa kufuatia kuushika mpira wakati timu yake ya taifa ilipokuwa ikicheza na Jamhuri ya Ireland katika harakati za kuwania nafasi kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo amejikuta katika mzozo mkubwa kutokana na kitendo chake hicho ambacho kiliisaidia Ufaransa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa kulazimisha sare ya bao moja kwa moja.

Henry ametoa kauli hiyo alipohojiwa na gazeti la Ufaransa la L'Equipe ambapo amesema huenda ikamlazimu kufanya hivyo kufuatia maneno mengi yanayosemwa juu yake.

No comments:

Post a Comment