KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 27, 2009

UBAGUZI MPAKA LINI?


Kiungo wa kimataifa toka nchini Mali na klabu ya Juventus ya nchini Italia Mohamed Sissoko ametaka kutazamwa upya kwa adhabu wanayopewa mashabiki ambao wamekua wakionyesha vitendo vya ubaguzi wa rangi viwanjani.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool ametaka hatua hiyo itazamwe upya kufuatia mshabiki wa klabu yake ya Juventus kuimba wimbo wa kuonyesha vitendo hivyo dhidi yake baada ya kufungwa na na klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya.

Kiungo huyo amesema mashabiki wa klabu ya Juventus mara kadhaa wamekua akionyesha tabia ya ubaguzi wa rangi ambapo pia walishawahi kufanya hivyo kwa mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan Mario Balotelli.

1 comment:

  1. Kwa hilo bwana Sissoko sio kwawachezaji tu,bali wazungu bwana kwa mtu mweusi ni mambo mengine.Ukija kuzungukia jinsi wanavyomchamba rais wa USA na sio mweusi pyuwa,,je na sisi tunaofanana na vyungu je?hamna jinsi haya ni matatizo ambayo hayatapata dawa hata siku moja.

    ReplyDelete