KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 18, 2009

WENGER ATOA USHAURI.

Meneja wa klabu ya Arsenal ARSENE WENGER anaamini kiungo wa kimataifa Patrick Vieira anatakiwa kuchukua uamuzi wa kuondoka katika klabu yake ya sasa Inter Milan katika dirisha dogo la usajili endapo anahitajia kurejea kwenye klikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Arsene wenger amemshauri kiungo huyo kufanya hivyo huku akikanusha taarifa za yeye kuwa tayari kumrejesha kwenye kikosi chake kama ilivyozungumza siku kadhaa zilizopita.

Vieira mwenye umri wa miaka 33 amepoteza nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kushindwa kupata nafasi ya kikosi cha kwanza chini ya kocha wa Inter Jose Mourinho.
Wenger amesema ili mchezaji aweze kucheza katika fainali za kombe la dunia lazima apate nafasi ya kucheza kila mara katika klabu yake hivyo ni vigumu kwa kiungo huyo kujihakikishia nafasi hiyo endapo Ufaransa itafanikiwa kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya timu ya taifa ya Ireland ili iweze kucheza fainali za kombe la dunia.

Amesema endapo Viera atasikiliza ushauri wake kuna uwezekano mkubwa wa kucheza katika kombe la dunia za mwaka 2010.

Lakini alipoulizwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kama anaweza kumrejesha kiungo huyo katika klabu ya Arsenal, Wenger amesema anaweza kucheza kamari kwa kuweka fedha kwa sababu hadhani kama Viera atarejea nchini Uingereza .

No comments:

Post a Comment