KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 16, 2009

NFF YAFIKIRIA KUMALIZA ZENGWE MAPEMA.


Shirikisho la soka la Nigeria (NFF) limesema lipo tayari kumaliza suala la marupurupu ya wachezaji wake watakaopshiriki fainali za Kombe la Dunia mapema zaidi kabla patashika hazijaanza mwakani.

NFF linakusudia kukamilisha masuala yote yanayohusu fedha kwa wakati muafaka ili kusiwe na jambo litakalovuruga maandalizi.

Mwaka 1998 wakati wa fainali za Kombe la Dunia timu ya Nigeria iliingia katika mzozo mkubwa wa wachezaji kudai marupurupu yao.

Shirikisho la soka Duniani Fifa limetangaza kutoa msaada wa fedha dola milioni 1 kwa kila timu itakayoshiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Hatua hiyo imeifanya NFF kuamua kufanya mazungumzo na wachezaji wa timu yao ya taifa ya Super Eagles mapema kuhusu posho zao.

No comments:

Post a Comment