Meneja wa klabu ya Liverpool Rafa Benitez amefanya mazungumzo na kiungo wake wa kimataifa toka nchini Argentina Javier Mascherano kuhusu hatma yake katika klabu hiyo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuihama Liverpool na kujiunga na klabu ya Barcelona mwishoni mwa msimu huu.
Baada ya mazungumzo hayo Benitez amesema Mascherano ana furaha kuendelea kubaki Anfield na mazungumzo yanaandaliwa kwa ajili ya kumuongezea mkataba.
Mbali na Mascherano Benitez pia ana mipango ya kumuongezea mkataba kipa wake Pepe Reina.
Benitez amesema kipa huyo ni mfano wa wachezaji wengine kumuiga kutokana na kujituma na kuwa na furaha kuendelea kubaki Anfiled.

No comments:
Post a Comment