Katika hali ya kushangaza mshambuliaji Wayne Rooney amesema alishindwa kufuatilia upangaji wa makundi wa fainali za kombe la dunia uliofanyika nchini Afrika kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya kupitiwa na usingizi.
Ronney ambaye kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja alipitiwa na usingizi akiwa kambini na wachezaji wenzake katika hotel moja mjini Manchester kwa ajili ya mchezo uliochezwa dhidi ya klabu ya West Ham mwishoni mwa juma lililopita.

Rooney mwenye umri wa miaka 24 amesema alipewa taarifa na wachezaji wenzake baada ya kupitiwa na usingizi wakati akiendelea kufuatilia draw hiyo kupitia runinga .
Aidha mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza amesema alipitiwa na usingizi kutokana na kukesha mara kwa mara akimsaidia mkewe kulea mtoto nyakati za usiku .
Mpaka sasa Rooney na mkewe hawataki kumuajiri mlezi wa mtoto wao aitwae Kai aliyezaliwa November 2 mwaka huu.
Mara baada ya kuelezwa jinsi makundi yalivyopangwa Rooney amesema haijui vizuri timu ya Algeria lakini ana matumaini kwamba kocha wao Capello atawapa malekezo kuihusu timu hiyo kabla ya mchezo .
Katika draw hiyo Uingereza imepangwa katika kundi C pamoja na timu za USA, Algeria na Slovenia .
No comments:
Post a Comment