
Wakati makundi ya fainali za kombe la dunia yakitarajiwa kupangwa Disemba 04 huko mjini Cape Town nchini Afrika kusini, gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Carlos Alberto Torres amesema haipi nafasi timu hata moja toka bara la Afrika katika harakati za kutwaa ubingwa wa fainali hizo zitakazochezwa mwaka 2010.
Torres amesema ushawishi huo wa kutodhani timu za Afrika hazitoweza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo anaupata kufuatia kutoawamini ipasavyo wachezaji toka barani Afrika ambao mara kadhaa wamekuwa wakishindwa kufanya kweli kwenye fainali hizo kubwa ulimwenguni kote.
Torres amesema mpaka sasa bado hajaona timu hata moja toka barani Afrika ambayo inampa mshawasha na kuihofia huenda ikatwaa ubingwa wa fainali hizo, hivyo karata yake anaendelea kuiangusha katika mataifa toka nje ya bara hilo ambayo yatashiriki fainali za mwaka 2010.
Amesema timu za taifa za Cameroon pamoja na Senegal zote kwa pamoja zimeshaonja ladha ya hatua ya robo fainali ya fainali za kombe la dunia lakini zilishindwa kuonyesha uwezo wa kutosha wa kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Ikumbukwe kuwa Mwaka 2010 bara la Afrika litawakilishwa na timu za mataifa sita ambayo ni Afrika kusini , Ivory Coast, Cameroon, Algeria,Nigeria pamoja na Ghana.
Hilo ndo tatizo la wazungu,,
ReplyDeleteInamaana huyu mshamba ameshaona kwamba timu za afrika hazina uwezo kufika fainali?Kwanini timu vigogo zimeponea chupuchupu kwakuingia kombe hilo?Mimi wala sikubaliani naye,sema tu ni kutokana na jinsi wazungu wanavyotudhalau siku zote kutokana jinsi tunavyoshinda kwao kuwaomba mahitaji flani flani.