KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 14, 2009

WENGER ATAMBA KUREJEA KATIKA MBIO ZA UBINGWA.


Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Liverpool meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kikosi chake kimerejea katika mbio za ubingwa msimu huu.

Wenger amesema mwanya uliopo wa point sita kati yao na Chelsea bado unaweza kuzibwa na vijana wake hivyo matumaini ya kutwaa ubingwa kwake bado yapo hai baada ya kufifia majuma kadhaa yaliyopita.

Arsene Wenger pia amemwagia sifa kem kem nahodha na kiungo wake wa kimataifa toka nchini Hispania Cesc Fabregas kufuatia kiwango cha soka alichokionyesha katika mchezo huo wa jana huku akieleza kwamba kiwango cha mchezaji huyo kilichangia kupatikana kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja mbele ya Liverpool.

Katika mchezo huo The Gunners walikwenda mapumziko huku wakiwa nyuma kwa bao moja na waliporejea katika kipindi cha pili walifanikiwa kusawazisha kupitia bao la kujifunga lililopachikwa wavuni na Glen Johnson huku Andrey Ashavin akipachika msumari wa pili kwa shuti kali.

No comments:

Post a Comment