KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 7, 2009

TP MAZEMBE WAWEKA MALENGO MAKUBWA.



Klabu bingwa barani afrika kutoka DR Congo TP Mazembe inaamini inaweza kuwa na mafanikio kuliko klabu nyingine barani afrika katika michuaono ya klabu bingwa duniani .

Mabingwa hao wa bara la Afrika wanataraji kucheza na klabu ya Pohamba Steelers kutoka Korea Kusini katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo December 11 huko katika falme za kiarabu .

Iwapo watafanikiwa katika mchezo huo watacheza na klabu ya Estudiantes de La Plata kutoka nchini Argentina katika hatua ya nusu fainali.

Kocha wa klabu hiyo mfaransa Diego Garzitto amesisitiza kuwa wana matumaini ya kufanya vizuri kuliko klabu ya Al Ahly ya nchini Misri waliomaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya klabu bingwa duniani msimu uliopita .

Mazembe, ambao kwa sasa wameweka kambi katika nchi ya Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo klabu bingwa dunia huenda wakamkosa mshambuliaji wao anayeweza kuhamia barani ulaya Tresor Mputu Mabi.

Mputu ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo timu hiyo ni mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa soka barani Afrika (BBC African Footballer of the Year award).

Hata hivyo msemaji wa klabu hiyo Eddy Kabhelu amesema hawana wasiwasi wowote iwapo Mputu ataihama klabu hiyo kwani tayari wana wachezaji wengine watakaochukua nafasi yake.


No comments:

Post a Comment