
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger amesema katu hatotuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Mario Balotelli.
Meneja huyo wa klabu ya Arsenal ametoa kauli hiyo baada ya kuhusishwa na taarifa za kuwa mbioni kumsajili Balotelli mwezi januari katika dirisha dogo la usajili.
Meneja huyo amesema licha ya kukiri kwamba yu mbioni kumsaka mshambuliaji mwingine ambae ataziba mwanya wa Robin Van Persie alie majeruhi kwa sasa, hana pupa ya kumsajili Balotelli kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment