KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 8, 2009

TUNAHITAJI USAIDIZI.


Nahodha wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas amekiri kikosi cha The Gunners hakina budi kuongezewa mshambuliaji mahiri katika dirisha dogo la usajili mwezi januari mwaka 2010.

Kiungo huyo amekiri huko kufuatia mwenendo wa kikosi chao ambacho majuma mawili yaliyopita kiliyumba katika michezo miwili ya ligi kuu sambamba na kutolewa kwenye michuano ya kombe la ligi kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri na Manchester City kabla ya kupata ushindi mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Stoke City.

Amesema Arsenal inamiliki mpira kwa muda mrefu lakini haina mtu mwenye uwezo wa kwenda mbele kupambana na walinzi wa timu pinzani zaidi ya anavyofanya mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Mexico Carlos Vela.

Fabregas amesema kikosi chao kinamuhitaji mshambuliaji kama Didier Drogba wa Chelsea ambae huonyesha umahiri mkubwa wa kukabiliana na safu ya ulinzi ya timu pinzani na kufikia hatua ya kupachika mabao.

1 comment:

  1. Kumbe we mtoto unamacho kabisaa! Kwani Drogba ni hatali kila timu pinzani lazima anaponyoka tu,nakupachika goli.

    ReplyDelete