Mabingwa wa soka wa dunia, wa mwaka 1998 Ufaransa hawapo kwenye bakuli maalum la kwanza ambalo litaziewesha timu za taifa kuongoza katika utaratibu wa upangaji wa makundi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 ambapo hatua hiyo ya upangaji wa makundi itafanyika Disemba 4 mjini Cape Town Afrika kusini.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA Jerome Valcke ametoa ufafanuzi wa nchi hiyo kutokuwepo kwenye bakuli hilo ambapo amesema sababu kubwa iliyowaondoa Ufaransa katika utaratibu huo ni kushirikishwa mwenyeji wa fainali hizo pamoja na bingwa mtetezi.
Utaratibu huo unaziondoa timu za taifa za Ufaransa pamoja na Ureno ambazo kiutaratibu wa viwango vya soka duniani zilistahili kuwepo katika bakuli hilo lakini kwa kigezo kilichotolewa na katibu wa FIFA hakuna budi kwa nchi hizo kupelekwa katika mabakuli mengine.
Kufuati utaratibu huo timu za taifa ambazo zitatengeneza makundi manane ya fainali za kombe la dunia ni wenyeji Afrika kusini South Africa, bingwa mtetezi Italy, Argentina, Brazil, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi pamoja na na Hispania ambazo zipo kwenye bakuli la kwanza.
Katika bakuli la pili zipo timu za taifa za Australia, Honduras, Japan, Mexico, New Zealand, North Korea, South Korea pamoja na Marekani.
Bakuli la tatu kuna timu za Algeria, Cameroon, Chile, Ghana, Ivory Coast, Nigeria, Paraguay pamoja na Uruguay.
Na katika bakuli la nne kuna timu ya taifa ya Denmark, France, Greece, Portugal, Serbia, Slovakia, Slovenia and Switzerland.
No comments:
Post a Comment