KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, March 12, 2010

ARSENE AWAPASHA HABARI MADRID.


Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameutaka uongozi wa klabu ya Real Madrid kuachana nae katika harakati zao za kumtafuta mbadala wa meneja wao wa sasa Manuel Pellegrini.


Wenger ameupasha habari uongozi wa the Merengues, kufuatia kuhusishwa na taarifa za kuwa miongoni mwa mameneja wanaopewa nafasi za juu kuelekea huko St Bernabeu.


Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ufaransa amevieleza vyombo vya habari kwamba, kwa hivi sasa hafikirii kuondoka Emirates kutokana na mkataba wake kumbana hadi mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment