KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, March 6, 2010

DONOVAN KUREJEA NYUMBANI.


Harakati za klabu ya Everton za kutaka kuongeza muda wa mkataba wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Marekani na klabu ya Los angles Galax Landon Donovan zipo mbioni kugonga ukuta kufuatia kauli iliyoitolewa na meneja wa klabu ya LA GALAX Bruce Arena.


London Donovan ambae ni nahodha wa timu ya taifa ya Marekani tayari ameshaombewa nafasi ya kuendelea kusalia na huko Merseyside na meneja wake wa sasa David Moyes ambae ameonyesha namna ya kuukubali mchango wake ndani ya everton.


Ombi hilo la Moyes limetumwa huko nchini Mrekani, lakini hii leo meneja wa klabu ya LA Galax Bruce Arena amejibu kwa kusema kwamba ombi hilo la Moyes halitowezekana.

No comments:

Post a Comment