
Beki na nahodha msaidizi wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher amesema hatoakuwa na kinyongo endapo uongozi wa klabu yake ya sasa utashindwa kumpatia mkataba mpya wa kuendelea kusalia huko Anfield.
Carragher, ambae ni mmoja wa wachezaji waliokaa kwa muda merefu wakiwa na klabu ya Liverpool ameyasema hayo kufuatia mkataba wake wa sasa kuwa mbioni kumalizika huku kukiwa hakuna dalili zozote za kuanza kwa mazungumzo mpya ya kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema pamoja na hali halisi iliopo sasa ya kutoonyeshwa dalili za kusaini mkataba mpya, bado ataendelea na shughuli ya kuitumikia Liverpool kwa moyo wake wote.
No comments:
Post a Comment