
Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amesema kwa sasa anaamini atacheza katika kiwango chake baada ya kuwa katika mazingira magumu ya kuzomewa na mashabiki pale anapokua uwanjani.
John Terry ambae ana wakati mgumu wa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na rafiki wa zamani wa kike wa aliekua beki mwenzake wa klabu ya Chelsea Wayne Bridge ambae kwa sasa anaichezea klabu ya Man City, kwa kipindi cha majuma matatu yaliyopita alionekana kucheza chini ya kiwango na kupelekea The Blues kupoteza michezo yake dhidi ya Everton, Inter Milan pamoja na Man City.
No comments:
Post a Comment