
Meneja wa klabu ya Inter Milan Jose Mourinho huenda akaingia kwenye harakati za kujifikiria ajiunge na klabu ipi mwishoni mwa msimu huu kufuatia jina lake kujitokeza kwenye klabu mbali mbali za huko barani ulaya.
Mourinho anadhaniwa kuwa katika mlolongo huo kufuatia jina lake kujitokeza katika kinyang’anyiro cha kuziba nafasi ambayo huenda ikaachwa wazi na meneja wa sasa wa klabu ya Real Madrid Manuel Pelegrin.
Mbali na jina la meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno kujitokeza katika orodha ya klabu ya Real Madrid pia jina lake limejitokeza kwenye vilabu vya Liverpool pamoja na Manchester City vyote kutoka nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment