KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 25, 2010

KIKOSI CHA AUSTRALIA CHAZIDI KUPUNGUZWA.


Mshambuliaji wa klabu ya Middlesbrough ya nchini Uingereza Scott McDonald amekua miongoni mwa wachezaji watatu waliachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Australia kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia.

Mshambuliaji huyo ameachwa na kocha mkuu wa timu hiyo Pim Verbeek baada ya kuonyesha kiwango duni kwenye mchezo wa jana wa kujipima ubavu dhidi ya New Zealand ambao walikubali kibano cha mabao mawili kwa moja.
Sababu nyingine iliyomuondoa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kikosini ni kufuatia kukosa kupachika bao hata moja kwenye michezo 16 ya timu ya taifa aliyocheza.

Kuondolewa kwa mchezaji huyo kunamaanisha timu ya taifa ya Australia imesaliwa na washambuliajni watatu ambao ni Josh Kennedy, Harry Kewell pamoja na Nikita Rukavysya.

Wachezaji wengine aliotemwa na Pim Verbeek ni kiungo wa klabu ya Crystal Palace Nick Carle pamoja na beki Jade North .

No comments:

Post a Comment