
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello ameonyesha matumaini ya kumtumia kiungo wa klabu ya Man City Gareth Barry kwenye fainali za kombe la dunia huko nchini Afrika kusini.
Capello ameonyesha dhamira hiyo kufuatia kumpa kiungo huyo muda wa juma moja ili aweze kujiweka vyema licha ya kuuguza jeraha la kifundo cha mguu linalomkabili kwa sasa.
Kocha huyo wa kimataifa toka nchini Italia ametoa muda huo kwa Barry kwa lengo la kumfuatilia maendeleo yake kabla ya kutajwa kikosi cha wachezaji 23 mnamo June 1.
No comments:
Post a Comment