Nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas, hatimae amevunja ukimya na kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wake kuondoka ama kutokuondoka huko Emirates katika kipindi hiki cha usajili.
Fabregas amezungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Hispania ambayo inajiandaa na fainali za kombe la dunia.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema hivi karibuni alizungumza na meneja wake Arsene Wenger na kushauriwa aachane na taarifa za kujiunga na klabu ya Barcelona na badala yake afikirie ni namna gani ataisaidia timu ya taifa lake huko Afrika kusini.
Amesema mara kadhaa amekua akiulizwa juu ya kuhama kwake Arsenal na kutarajia kujiunga na klabu ya Barcelona lakini kabla ya kujibu amekua akisaka ushauri kwa Arsene Wenger anaemuheshimu kama baba yake mzazi.
Hata hivyo kiungo huyo aliejiunga na klabu ya Arsenal akiwa na umri wa miaka 16, amewataka waandishi wa habari kuacha kumuulizwa swali la uhamisho wa kutoa Arsenal kwenye Barcelona kwani maamuzi ya kuondoka ama kubaki yapo mikononi mwa babu huyo wa kifaransa.

No comments:
Post a Comment