Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Aruna Dindane ameihama klabu yake ya Portsmouth na kujiunga na klabu ya Lekhwiya ya nchini Qatar.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameihama klabu ya Portmouth huku akiacha kumbu kumbu ya kufunga mabao tisa kwenye michezo yote aliyocheza msimu wa mwaka 2009-10.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameihama klabu ya Portmouth huku akiacha kumbu kumbu ya kufunga mabao tisa kwenye michezo yote aliyocheza msimu wa mwaka 2009-10.
Dindane pia atakumbukwa huko Fraton Park kwa hatua ya kusaidiana na wachezaji wengine kuipelekea klabu ya Portsmouth kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la FA msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment