KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 27, 2010

BRAZIL WAWASILI AFRIKA NA RAISI WAO.


Baada ya kuwasili salama wa salmini kwenye ardhi ya bara la Afrika, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Carlos Caetano Dunga, amesema kikosi chake kipo tayari kwa fainali za kombe la dunia.

Dunga amesema pamoja na siku 14 kusalia kabla ya kipyenga kupulizwa kuashiriki fainali hizo kuanza huko nchini Afrika kusini, anaamini maandalizi anayoyafanya yanampa mwanya wa kusema wapo tayari.

Amesema pamoja na kuamini wachezaji wake wapo tayari bado anaamini fainali za kombe la dunia za mwaka huu zitakuwa na ushindani wa aina yake hivyo hana budi kulifikiria na hilo pia.

Kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Brazil hii leo kimewasili nchini Afrika kusini sambamba na raisi wa nchi hiyo Ignacio Lula Da Silva na kinatarajia kuja Tanzania kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na kisha kitacheza na timu ya Zimbabwe.

Timu ya taifa ya Brazil imepangwa katika kundi la saba lenye timu za taifa za Ivory Coast, ureno pamoja na Korea Kaskazini.

Timu nyingine iliyowasili nchini Afrika kusini tayari kwa mshike mshike wa fainali za kombe la dunia ni timu ya taifa ya Australia ambayo inanolewa na Pim Verbeek.


Timu nyingine inayotajwa kuwasili huko nchini Afrika kusini mara baada ya Brazil na Australia ni Argentina iliyo chini ya Diego Armando Maradona.

No comments:

Post a Comment