KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 28, 2010

UEFA KUVIBANA VILABU.


Shirikisho la soka barani ulaya UEFA hii leo litazindua sheria mpya zitakazo vibana vilabu kutumuia kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya mapato yanayopatikana kwenye vilabu hivyo.

UEFA wanazindua sheria hizo baada ya muda wa miaka mitatu ambayo imetumika katika harakati za kutunga sheria hizo ambazo zitaidhinishwa wa kamati kuu ya shirikisho hilo.

Sheria hizo zitazuia vilabu kupata hasara kila mwaka na kuwazuia vibopa kuwekeza fedha nyingi kwa kununua wachezaji wapya.

Hata hivyo sheria hiyo itaviruhusu vilabu kutumia kiasi chochote cha pesa kununua wachezaji kama vina fedha za kutosha.

No comments:

Post a Comment