KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 27, 2010

PELLEGRIN out MOURINHO in.


Hatimae uongozi wa klabu ya Real Madrid umetangaza kumfungashia virago aliekua meneja wa klabu hiyo Manuel Pellegrini, alienza kibarua chake mwanzoni mwa msimu huu.

Akitangaza rasmi taarifa za kufungashiwa virago kwa meneja huyo, raisi wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amesema wamefiki maamuzi hayo kufuatia meneja huyo kushindwa kufikia malengo waliyokua wamejiwekea msimu uliopita.

Perez amesema msimu uliopita walijiwekea malengo ya kuwa mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na ulaya lakini Pellegerini alishindwa kufikia malengo hayo hivyo wameona ni bora kumsaka meneja mwingine.

Hata hivyo raisi huyo wa Madrid ameweka wazi suala la kuwa mbioni kumuajiri Jose Mourinho anaetajwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Real Madrid mara baada ya kuizawadia ubingwa wa ulaya Inter Milan mwishoni mwa juma lililopita huko St Bernabeu.

Perez amethibitisha hatua hizo mbele ya waandishi wa habari kwa kubainisha wazi kwamba Mourinho ndie meneja anaefaa katika utaratibu wa kuipa zawadi ya mafanikio klabu ya Real Madrid.

Wakati huo huo Manuel Pellegrin mwenye umri wa miaka 56, ameulaumu wazi wazi uongozi wa klabu ya Real Madrid huku akisema uongozi huo ulikuwa chanzo cha yeye kutokufikia malengo aliyowekewa.

Pellegrin amesema alipendekeza kwa uongozi huo suala la kutokuuzwa kwa Wesley Sneijder pamoja na Arjen Robben, lakini pendekezo hilo liliwekwa kapuni.

No comments:

Post a Comment