Uongozi wa chama cha soka nchini Ghana GFA umesema kiungo wa klabu ya Chelsea Michael Essien hatocheza fainali za kombe la dunia za mwaka huu zitakazounguruma huko nchini Afrika kusini.
GFA wametoa taarifa hizo kufuatia jeraha la goti la la kiungo huyo kutokupona kwa wakati kama ilivyokua inatarajiwa na wengi siku kadhaa zilizopita.
Taarifa hizo zimeongeza kuwa Michael Essien anatabiriwa kupona jaraha l la goti mwishoni mwa mwezi July na huenda asiuanze vyema msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza akiwa na klabu yake ya Chelsea.
Itakumbukwa kuwa Essien alitoneshwa jeraha lake la goti na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba kwenye fainali za mataifa ya Afrika zilizochezwa mwanzoni mwa mwaka huu nchini Angola.
katika fainali za kombe la dunia timu ya taifa ya Ghana imepangwa kwenye kundi la tatu lenye tikmu za Ujerumani, Australia pamoja na Serbia.
wakati huo huo timu zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia zimeendelea kujichua vikali kwa kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki ambapo uasiku wa kuamkia hii leo.

No comments:
Post a Comment