KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 27, 2010

OBI KWENDA UINGEREZA.


Kiungo wa klabu ya Chelsea John Obi Mikel anatarajia kujiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya timu ya taifa ya Nigeria iliopo nchini Uingereza siku ya ijumaa.

Mikel atajiunga na wenzake baada ya kuthibitika amepona jeraha lake la goti ambalo lilimpelekea kukosa michezo ya mwishoni mwa msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 mara atakapojiunga na wachezaji wenzake kambini ataanza mazoezi na huenda akawepo kwenye kikosi cha Nigeria ambacho kimesalia na michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia.

Katika mchezo wa kwanza Nigeria watacheza na timu ya taifa ya Columbia nchini Uingereza na baada ya hapo watacheza na Korea kusini mjini Johannesburg mnamo June 6.

Wakati huo huo zikiwa zimesalia siku 14 kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia shirikisho la soka ulimwenguni FIFA hii leo limetoa msimamo wa viwango vya ubora wa mataifa mbali mbali.

Katika viwango hivyo wenyeji wa fainali za kombe la Dunia Afrika kusini wamepanda kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 90 hadi ya 83.

No comments:

Post a Comment