KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 25, 2010

FABREGAS USIFANYE KOSA KAMA LANGU - HLEB.


Kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal Alexander Hleb amemtaka CESC FABREGAS kutothubutu kufanya kosa kama alilolifanya yeye alipojiunga na klabu ya Barcelona mwaka 2008.

Hleb amesema mara kadhaa amekua akiwasilina na nahodha huyo wa klabu ya Arsenal na kumueleza juu ya maamuzi yake anayotaka kuyachukua ya kurejea FC Barcelona.

Amesema amemshauri Fabrigas kuendelea kusalia emirates kwani yeye anaamini kikosi cha Arsenal kina uwezo wa kufanya makubwa msimu ujao kikiwa chini yake.

Itakumbukwa kuwa Alexander Hleb aliondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya Barcelona kwa kisingizio cha kufuata mafanikio, lakini alijikuta akikalishwa benchi hatua ambayo ilisababisha kiwango chake kushuka.

No comments:

Post a Comment