KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, May 23, 2010

Gerrard apania kung'ara A.Kusini.


BAADA ya kushindwa kuonesha makali yake katika kikosi cha Liverpool, kiungo Steven Gerrard amesema kuwa, anaamini atarejea katika kiwango chake cha kawaida na kuisaidia timu ya Taifa ya England kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Hivi karibuni Gerrard amekuwa akihusishwa na tetesi mbalimbali za kuwa, majira haya ya kiangazi ataitema klabu hiyo ya Anfield baada ya kupoteza imani na kocha Rafael Benitez.

Msimu uliopita, Reds ilimaliza Ligi Kuu ikiwa nafasi ya saba baada ya miezi 12 iliyopita kukaribia kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na kisha kutupwa nje ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya mapema.

Lakini, Gerrard (29), amepania kujaribu kutwaa taji hilo nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha kocha Fabio Capello na akawataka wachezaji wenzake wa England kufanya kweli ili kuhakikisha wanaondoka na taji hilo kubwa katika soka.

Akizungumzia matumaini yake hayo, kiungo huyo alisema: "Ulikuwa ni msimu mgumu kwangu na kwa Liverpool kwa sababu tulikuwa chini ya mafanikio," alisema Gerrard

"Hatukuweza kufikia malengo tuliyoyaweka mwanzoni mwa msimu, jambo ambalo limemuumiza kila mmoja, lakini kwa sasa tupo mahali hapa na England, ni muhimu masuala ya klabu tukayaweka pembeni," aliongeza Gerrard.


Alisema jambo ambalo ameliweka mbele yake ni kwenda katika fainali za Kombe la Dinia kufanya vizuri yeye na timu ya Taifa ya England.

"Jambo zuri ni kwamba, nakaribia kurejea katika kiwango changu ambacho nataka kuwepo.

No comments:

Post a Comment